KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 11, 2011

Fernando Torres SHAKANI KUCHEZA JUMAPILI !


Mshambuliaji kutoka nchini Hispania Fernando Torres huenda akakosa sehemu ya mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza ambapo klabu yake ya Chelsea itaanza kusaka ubingwa wa nchini humo kwa kucheza na Stoke city.

Fernando Torres amezusha hofu ya kukosa mchezo wa ufunguzi, kufuatia matatizo yalioyomfika akiwa katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Hispania dhidi ya mabingwa wa soka duniani mwaka 2006 Italia.

Mshambuliaji huyo alipoteza fahamu baada ya kugongana na mchezaji wa Italia, hatua ambayo ilipelekea kutolewa nje ya uwanja katika dakika ya 14, na kukimbizwa katika hospitali ya mji wa Bari.

Hata hivyo Fernando Torres, aliruhusiwa kutoka hospitali na kisha alijiunga na wachezaji wenzake ambao jana walimaliza mchezo kwa uchungu wa kufungwa mabao mawili kwa moja.

Wakati huo huo nahodha na beki wa Chelsea John Terry amesema kikosi chao kipo tayari kwa ajili ya kuanza kwa ligi huku akisifia ujio wa meneja mpya Andre villas Boas aliejiunga nao akitokea FC Porto miezi miwili iliyopita.

Amesema kila mmoja kikosini kwa sasa yupo tayari baada ya maandaliai ya msimu ambayo yalipelekea kufanya ziara barani Asia kabla ya kurejea barani Ulaya majuma mawili yaliyopita.

No comments:

Post a Comment