KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 30, 2011

Frankie Fielding AITWA KIKOSINI NA FABIO CAPELLO.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza, Fabio Capello amelazimika kumuita kikosini kipa wa klabu ya Derby County Frankie Fielding, kufuatia uhaba wa makipa.

unaokiandama kikosi chake ambacho kwa sasa kinajiandaa na mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za barani Ulaya dhidi ya Bulgaria mwishoni mwa juma hili.

Fabio Capello amelazimika kufanya hivyo, kufuatia kipa wa West Ham Utd Robert Green kutangaza kujiondoa kikosini kufautia sababu za kuwa majeruhi.

Robert Green, mapema hii leo alitarajiwa kujiunga na wachezaji wenzake kambini tayari kwa kuendelea na maandalizi, lakini cha kushangaza benchi la ufundi lilipokea taarifa za kutokufika kwake huku taarifa hiyo ikieleza amejiondoa.

Hii inakua ni mara ya kwanza kwa kipa Frankie Fielding mwenye umri wa miaka 23, kuitwa katika timu ya taifa ya Uingereza ya wakubwa, na mara ya mwisho alionekana katika majukumu ya kitaifa kwenye fainali za vijana za ulaya zilizofanyika nchini Denmark mwezi june mwaka huu.

Kwa mantiki hiyo sasa timu ya taifa ya Uingereza ambayo itasafairi hadi mjini Sofia kucheza mpambano wake dhidi ya Bulgaria, inakuwa na makipa watatu ambapo chaguo la kwanza ni kipa wa Man city Joe Hart chaguo la pili ni kipa wa Fulham ambapo kwa sasa anaeitumikia Ipswich Town kwa mkopo David Stockdale na chaguo la tatu ni Frankie Fielding.

No comments:

Post a Comment