KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 9, 2011

Gabriel Obertan ATUA NEWCASTLE UTD.


Newcastle Utd wamekamilisha usajili wa winga kutoka nchini Ufaransa Gabriel Obertan, akitokea Man Utd kwa ada ya uhamisho wa paund million 3.

Newcastle Utd wamekamilisha dili hilo kwa muda wa siku tatu ambapo mwishoni mwa juma lililopita waliripotiwa kuanza mazungumzo ya kumsajili winga huyo ambae alisajiliwa na Man utd mwaka 2009 akitokea Bordoux ya nchini Ufaransa.

Baada ya kukamilisha usajili huo Gabriel Obertan, alizungumza na waandishi wa habari na kueleza mustabaki wa maisha yake ndani ya Newcastle Utd ambapo amesema atajitahidi kwa kila hali kuhakikisha anafanya vyema na kufikia malengo yaliyowekwa klabuni hapo.

Amesema amekwenda St James Park akiwa na uchu wa kucheza soka pamoja na kuiwezesha Newcastle utd kufanya vyema katika msimu mpya wa ligi hivyo wametoa tahadhari kwa vilabu pinzani hususan Arsenal ambao watafungua ligi kwa kupambana na The Magpies.

Alan Pardew meneja wa Newcastle utd amesema kwao ni habari njema na pia wanaamini ujio wa Obatan utakisaidia kikosi chake katika msimu wa ligi wa mwaka 2011-12.

Gabriel Obertan amesaini mkataba wa miaka mitano ambao utamuweka huko Sta Jemes Park hadi mwaka 2016.

Pia anakua mchezaji wa tano kusajiliwa na Newcastle Utd katika kipindi hiki ambapo alitanguliwa na wachezaji kama Yohan Cabaye, Demba Ba, Sylvain Marveaux pamoja Mehdi Abeid.

No comments:

Post a Comment