KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 9, 2011

GAME YA NIGERIA NA GHANA YAFUTWA.

Mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya Nigeria dhidi ya timu ya taifa ya Ghana uliokua umepangwa kufanyika hii leo nchini Uingereza kwenye uwanja wa Vicarage Road umeahirishwa.

Mchezo huo uliokua na malengo ya kuziandaa timu hizo kabla ya kuendelea kwa michezo ya awali ya fainali za mataifa ya bara la Afrika itakayoendelea mwezi ujao, umeahirishwa kufuataio zogo linaloendelea jijini London nchini Uingereza kati ya wananchi dhidi ya jeshi la polisi.Tayari timu zote zilishafika jijini London na bado haijaelezwa ni lini mchezo huo utachezwa na mpaka sasa wachezaji wa timu hizo wameshaanza kurejea katika vikosi vya klabu zao za barani Ulaya huku wale wanaocheza soka barani Afrika wakitarajia kuongozana na viongozi kurejea nyumbani.


Hata hivyo shirikisho la soka nchini Nigeria limeahidi kutoa maelezo zaidi juu ya mchezo huo, ambao utapangiwa tarehe nyingine.

No comments:

Post a Comment