KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 26, 2011

Gary Cahill AZUSHA VITA YA MANENO.


Klabu ya Bolton Wanderers wamethibitisha kuikataa ofa ya klabu ya Arsenal iliyomlenga beki wa kati kutoka nchini Uingereza Gary Cahill.

Bolton Wanderers wameikataa ofa hiyo kutoka jijini London kwa madai haikidhi haja ya kiasi cha fedha kinachohitajika huko Reebok Stadium kwa ajili ya kumpa ruhusa Garry Cahill kuondoka.

Meneja wa Bolton Wanderers Owen Coyle amesema Arsenal waliwasilisha ofa yao ya paund million 7, ambayo haiendani na matakwa ambayo tayari yameshawekwa wazi na mwenyekiti wake Phil Gartside ambae anataka zaidi ya kiasi hicho.

Hata hivyo Owen Coyle, amesema yu radhi kumuachia beki huyo kuondoka kutokana na mkataba wake wa sasa kutarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu na kuna dalili za kugoma kusaini mkataba mpya.

Hii si mara ya kwanza kwa Arsenal kufeli katika suala la kutaka kumsajili beki huyo mwenye umri wa miaka 25, kwani tayari walishafanya hivyo zaidi ya mara moja siku kadhaa zilizopita.

Mbali na beki huyo, pia Arsenal wanahusishwa na taarifa za kutaka kumsajili beki wa kati wa klabu ya Everton Phil Jagielka ambae nae ofa yake imeshakataliwa na viongozi wa The Tofees kwa madai haikidhi matakwa yao.

Clistopher Samba beki kutoka Congo Brazzaville pamoja na klabu ya Blackburn Rovers, nae yupo katika utaratibu wa kusajiliwa na washika bunduki wa Ashburton grove Arsenal ambao kwa sasa wanahangaika kukiboresha kikosi chao.

Wakati huo huo meneja wa Arsenal Arsene wenger amekanusha taarifa za kuwasilishwa kwa ofa ya paund million saba ambapo amesema hakuna ukweli wowote juu ya suala hilo zaidi ya kutaka kuchafuliwa katika sera yake ya usajili.

Amesema anachotambua kwa sasa Bolton Wanderers wapo tayari kumuuza Garry Cahill na wao wamewasilisha ofa ambayo itakuwa wazi mara baada ya mazungumzo kukamilishwa.

No comments:

Post a Comment