KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 18, 2011

Gerard Pique AMTUHUMU MOURINHO KWA KUHARIBU SOKA LA HISPANIA.

Beki wa mabingwa wa soka barani ulaya pamoja na nchini Hispania FC Barcelona Gerard Pique ametuhumu vikali meneja wa Real Madrid Jose Mourinho kwa kusema amekuwa chanzo cha kuharibu ladha ya soka nchini humo.

Gerard Pique ametoa tuhuma hizo ikiwa ni muda mchache mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa pili wa hatua ya fainali wa Spanish Super Cup uliochezwa usiku wa kuamkia hii ambapo The Galacticos walikubali kisago cha mabao matatu kwa mawili na kutimiza idadi ya kufungwa jumla ya mabao matano kwa manne.

Amesema Jose Mourinho ni mtu ambae amebadilisha mazingira ya soka nchini Hispania hasa zinapokutana timu hizo mbili katika michuano tofauti ambapo mpaka mwisho wa mchezo huwa hapakosekani fujo ambazo mara nyingine husababishwa na yeye kama meneja.

Amesema kabla ya kuja kwa meneja huyo kutoka nchini ureno timu hizo mbili zilionyesha mchezo wa kiungwana na wachezaji walionyeasha mapenzi baina yao lakini hii leo mambo yamekua tofauti huku sehemu ya kuchezea ikigeuzwa uwanja wa vita.

Katika mchezo wa jana picha za televisheni zilimuonyesha Jose Mourinho akimsukuma na kumfinywa jichoni meneja msaidizi wa FC Barcelona Tito Vilanova na kitendo hicho kilijitokeza baada ya purukushani zilizoibuka kufuatia rafu mbaya aliyochezewa Cesc Fabregas na beki wa pembeni wa real Madrid Marcelo.

Jose Mourinho toka alipowasili huko Estadio Stantiago Bernabeu amekua katika wakati mgumu pale unapofika mchezo dhidi ya mahasimu wake Fc Barcelona ambapo asilimia kubwa upande wake huonekana kukosa nidhamu ya kutosha.

Wakati huo huo Jose MOURINHO alionekana kwa mara ya kwanza toka mwishoni mwa juma lililopita akiingia katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alisikika akiwakandia wapinzani wake FC Barcelona kwa kusema kikosi cha Real Madrid kiliekea Camp Nou kucheza soka nasi kujiangusha kama ilivyokuwa na wachezaji wengine.

Mourinho amezungumza maneno hayo ikiwa ni saa chache baada ya kumsukuma na kumfinya machoni meneja msaidizi wa Barcelona Tito Vilanova ambapo mpaka sasa haijafajhamika nini sababu ya kufanya hivyo.

Amesema kiujumla kikosi chake kilionyesha mchezo mzuri wakati wote lakini alichukizwa na kitendo cha vijana wanaokota mipira kuondolewa uwanjani wakati wa kipindi cha pili.

Jose Mourinho amedai kwamba mpango huo hakupendezwa nao hata kidogo hasa ikizingatiwa umefanywa na timu yenye heshima kubwa duniani na matokeo yake ameutafsiri kama hatua ya kinyume na timu inayokosa uzoefu.

No comments:

Post a Comment