KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 9, 2011

Ibrahim Teteh Bangura AHAMIA NCHINI UTURUKI.



Mshambuliaji kutoka nchini Sierra Leone Ibrahim Teteh Bangura amekamilisha taratibu za kujiunga na klabu ya nchini Uturuki Bursaspor, akitokea nchini Sweden alipokua akiitumikia AIK Solna.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amejiunga na Bursaspor kwa mkataba wa miaka mitatu ambao utamuweka huko nchini Uturuki hadi mwaka 2014.

Hata hivyo ada ya uhamisho wa Ibrahim Teteh Bangura haijawekwa wazi kufuatia makubaliano ya viongozi wa vilabu hivyo kuafikiana suala hilo na kulifanya kuwa siri.

Ibrahim Teteh Bangura amezungumza na shirika la utangazaji la nchini Uingereza BBC na kuelezea furaha yake ya kuelekea nchini Uturuki ambapoa mesema amefarijika sana na uhamisho uliofanywa na sasa kilichosalia ni kuonyesha uwezo ambao utaisaidia klabu yake mpya.

Amesema alikua na wakati mzuri sana alipokua nchini Sweden, na aliyapenda sana mazingira ya AIK Solna, lakini alikua hana budi kukubali kubadili mazingira ya soka lake ambayo hii leo yamempeleka nchini Uturuki.

Akiwa na klabu ya AIK Solna Teteh Bangura, alifanikiwa kupachika mabao 15 katika michezo 17 aliyocheza msimu uliopita hatua ambayo ilikua chanzo cha kuanza kufuatiliwa na viongozi wa Bursaspor.

Mshambuliaji huyo, alisajiliwa na AIK Solna mwezi januari mwaka huu akitokea katika klabu ya ligi daraja la pili nchini Sweden Koping FF ambapo huko alicheza michezo 11 na kufunga mabao 12.

Msimu uliopita Bursaspor walimaliza katika nafasi ya tatu kweye msiammo wa ligi kuu ya soka nchini Uturuki hivyo kusajiliwa kwa Ibrahim Teteh Bangura ni kutaka kurekebisha makosa yaliyojitokeza.

No comments:

Post a Comment