KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 1, 2011

Javier Pastore AKARIBIA JIJINI PARIS.


Klabu ya Paris St Germain, inaripotiwa kuwa katika harakati za mwisho za kumsajili kuingo mchezeshaji kutoka nchini Argentina pamoja na klabu ya Palermo Javier Pastore ambae pia alikua akiwaniwa na Chelsea.

Mjumbe wa bodi ya PSG Nasser Al-Khelaifi amenukuliwa na vyombo vya habari nchini Ufaransa akitoa taarifa za mipango ya kusajiliwa kwa kiungo huyo ambae anadhaniwa huenda akaleta mabadiliko msimu ujao.

Amesema wamefurahishwa na mipango inavyokwenda kwa sasa na wanaimani wakati wowote Javier Pastore atakua mchezaji wao halali.

Wakati tambo hizo zikitolewa mjini Paris, huko nchini italia raisi wa klabu ya Palermo Maurizio Zamparini nae amethibitisha kuendelea vyema kwa mazungumzo kati yao na viongozi wa Paris St Germain ambao toka mwanzoni mwa juma lililopita wamekuwepo nchini humo.

Amesema katika makubaliano waliyofikia, ni suala la uhamisho wa mchezaji huyo ambalo linaigharimu PSG kiasi cha paund million 37.5.

PSG wamekua na nguvu ya kukisuka upya kikosi chao kufuatia ujio wa wawekezaji kutoka famle za kiarabu ambao wamepania kufanya mapinzudi kwenye soka la nchini Ufaransa.

Wawekezaji hao kutoka nchini Qatar pia wameshamuajiri kazi aliekua meneja wa klabu za Inter Milan pamoja na AC Milan za nchini Italia Leonardo, pamoja na kuwasajili viungo Mohamed Sissoko kutoka Juventus pamoja na Salvatore Sirigu kutoka Palermo.

No comments:

Post a Comment