KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 9, 2011

Javier Pastore APASUA UKWELI ULIOMPELEKA UFARANSA.

Javier-PASTORE.png Kiungo kutoka nchini Argentina Javier Pastore ametoa sababu za kukubali kusajiliwa na klabu yenye utajiri kwa sasa Paris St Germain na kukataa kujiungana klabu nyingine zilizokua zikimuwania katika kipindi hiki ikiwemo klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza.

Javier Pastore ambae mwishoni mwa juma lililopita alikamilisha usajili wa kujiunga na klabu hiyo ya mjini Paris akiitokea Udanise ya nchini Italia, amesema sababu kubwa iliyomvutia na kukubalia kujiunga na PSG, ni muonekano mpya wa kikosi cha klabu hiyo iliyopania kufanya mapinduzi ya soka la nchini Ufaransa msimu huu.

Amesema utaratibu wa usajili uliofanywa na viongozi wa klabu hiyo, ulimshawishi kufikia maamuzi ya kujiunga na PSG huku akiamini atakua mmoja wa wachezaji watakaofikia malengo yaliyowekwa klabuni hapo.

Hata hivyo kiungo huyo aliekamilisha usajili kwa ada ya uhamisho wa Euro million 42 ambazo ni sawa na ( Paund million 36.5) amewashukuru viongozi wa vilabu vingine vilivyokua vikimuwania kwa kuonyeha juhudi za kutaka kumsajili hatua ambayo ameitafsiri kama sehemu ya muonekano wa kipaji chake anapokua uwanjani.

Javier Pastore anakua mchezaji wa sita kusajiliwa na Paris St Germain katika kipindi hiki ambapo kabla yake walisajiliwa wachezaji kama Jeremy Menez, Salvatore Sirigu, Mohamed Sissoko, Kevin Gameiro pamoja na Blaise Matuidi.

Licha ya kujipanga kufanya vyema msimu huu PSG mwishoni mwa juma lililopita walianza vibaya michuano ya ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa, baada ya kukubalia kisago cha bao moja kwa sifuri kutoka kwa Lorient.

No comments:

Post a Comment