KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 26, 2011

JINAMIZI LA Luca Modric LAENDELEA KUIANDAMA SPURS.


Meneja wa Tottenham Hotspurs Harry Redknapp bado anaendelea kusumbuliwa na mzuka wa kuondoka ama kubaki kwa kiungo kutoka nchini Croatia Luka Modric ambae anahusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na majirani zao Chelsea.

Harry Redknapp amesema anaamini kiungo huyo atasalia klabuni hapo na kesho anatarajia kumtumia katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Manchester City ambao watafunga safari hadi White Hart lane.

Amesema matumaiani ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, kubaki klabuni hapo yalionekana mara baada ya kikao kilichomuhusisha Luca Modric pamoja na mwenyekiti wa klabu Daniel levy ambapo kubwa walililokubaliana ni kucheza katika mchezo wa kesho.

Amesema mbali na makubaliano hayo pia watu hao wawili wameafikiana vitu vingi ambavyo anaimani vitakamilishwa kwa wakati na mwisho wa siku mashabiki wa Spurs wataendelea kumuona Modric akijivinjari katika viwanja wa kaskazini mwa jiji la London.

Katika mchezo wa ligi uliopita ambapo Spurs walikubali kisago cha mabao matatu kwa sifuri kutoka kwa mabingwa watetezi Man Utd, Luca Modric aligoma kujumuishwa kikosini kwa kushinikiza suala lake la kuuzwa klabuni hapo liharakishwe, ambapo hata hivyo utaratibu huo ulikanushwa vikali na Harry Redknapp, baada ya kukaririwa akisema kuwa mchezaji huyo hakuwa vizuri kisaikolojia.

Luca Modric toka mwanzoni mwa harakati za usajili amekua akihusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na klabu ya Chelsea ambayo imekua ikiongeza dau la kutaka kufanya hivyo hadi kufikia paund million 30.

No comments:

Post a Comment