KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 12, 2011

Jose Enrique AJIUNGA NA LIVERPOOL.

Majogoo wa jiji Liverpool wamekamilisha usajili wa beki wa pembeni Jose Enrique akitokea Newcastle United.

Beki huyo kutoka nchini Hispania amekamilisha usajili huo, baada ya kufanyiwa vipimo vya afya jana huko Anfiled, huku Liverpool wakikubali kutoa kiasi cha paund million 6 kama ada ya uhamisho wake kutoka St james Park.

Jose Enrique mwenye umri wa miaka, 25 amesema kukamilishwa kwa uhamisho wake kutoka Newcastle utd hadi huko Anfiled kunafungua ukurasa mpya wa maisha yake katika soka ambapo anaamini hatua hiyo itamuwezesha kucheza soka zaidi ya alivyokua siku za nyuma.

Amesema ni faraja kubwa kwa mchezaji kama yeye kujiunga na klabu kubwa kama Liverpool, na sasa kilichosalia ni kurejesha fadhila kwa viongozi pamoja na mashabiki wa The Reds waliompokea kwa mikono miwili.

Kusajiliwa kwa beki huyo, kunamaanisha ataziba nafasi iliyoachwa wazi na Paul Konchesky aliuzwa kunako klabu ya Leicester City, huku beki mmoja kati ya Emiliano Insua aliepelekwa kwa mkopo Galatasaray ama Fabio Aurelio akitegemea kuuzwa katika kipindi hiki.

Jose Enrique anajiunga na wachezaji wengine waliosajiliwa na Liverpool toka mwezi June ambapo miongoni mwa wachezaji hao ni viungo kutoka nchini uingereza Stewart Downing pamoja na Jordan Henderson, kipa kutoka nchini Brazil Alexander Doni pamoja na kiungo kutoka nchini Scotland Charlie Adam.

Licha ya kuingia katika orodha ya wachezaji hao waliosajiliwa katika kipindi hiki, pia Jose Enrique anakuwa mchezaji wa saba kusajiliwa na meneja wa Liverpool King Kenny Dalglish toka alipokabidhiwa maradaka mwishoni mwa mwaka jana.

No comments:

Post a Comment