KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 15, 2011

Jose Mourinho AWAKIMBIA WAANDISHI.

Meneja wa Real Madrid Jose Mourinho, usiku wa kuamkia hii leo aliwakwepa waandishi wa habari kwa kutokwenda katika chumba cha mikutano na badala yake alimtuma msaidizi wake Aitor Karanka kufanya hivyo.

Jose Mourinho anadhaniwa kufanya maamuzi hayo, kufuatia hofu ya kuepuka maneno makali ambayo huenda yangemtoa kama ilivyokua katika mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Barcelona msimu uliopita.

Kitendo hicho kilionyeshwa na meneja huyo kutoka nchini Ureno mara baada ya kumaliza kwa mchezo wa kwanza wa kuwania ubingwa wa Super Cup ambao uliwakutanisha Real Madrid dhidi ya Fc Barcelona huko Estadio Stantiago Bernabeu usiku wa kuamkia hii leo.

Katika mkutano huo wa waandishi wa habari, meneja msaidizi wa Real Madrid Aitor Karanka aliulizwa kwa nini bosi wake ameingia mitini, na alijibu kuwa huo ni utaratibu waliojipangia hivyo hashangazwi na yeye kutoa taarifa za tathmini ya mchezo huo ambao ulimalizika kwa timu hizo kufunga mabao mawili kwa mawili.

Kama itakumbukwa vyema maneno makali yaliyotolewa katika mkutano na waandishi wa habari msimu uliopita yalipelekea, shirikisho la soka barani ulaya UEFA kumuadhibu, Jose Mourinho ambae alidai Fc Barcelona wamekua wakipendelewa wazi wazi, na pengine huenda walikua wanatumia kivuli cha waliokua wanawafadhili shirika la kuhudumia watoto lilio chini ya umoja wa mataifa UNICEF.

Mchezo wa pili wa Super Cup kati ya Real Madrid dhidi ya Fc Barcelona utachezwa juma lijalo katika uwanja wa Camp Nou huko mjini Barcelona.

No comments:

Post a Comment