KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 25, 2011

Jose Mourinho BADO ANAKUBALIKA KWA MASHABIKI.

Licha ya kuanza kufanyiwa uchunguzi wa sakata la kumskuma na kumfinya jicho meneja msaidizi wa mabingwa wa soka nchini humo FC Barcelona Tito Vilanova, usiku wa kuamkia hii leo meneja wa Real Madrid Jose Mourinho alipokelewa kwa shangwe na mashabiki waliohudhuria Estadio Stantiago Bernabeu kushuhudia mchezo wa kirafiki dhidi ya Galatasaray.

Jose Mourinho, alipokelewa kwa furaha na mashabiki hao baada ya kutoka katika vyumba vya kubadilishia kabla ya mchezo huo wa kirafiki haujaanza kupigwa, hatua ambayo imetafsiriwa bado anahitajika klabuni hapo.

Siku mbili zilizopita Jose Mourinho, alionyesha kukasirishwa na tuhuma zinazomuandana na kufikia hatua ya kuwataka radhi mashabiki wa soka nchini Hispania kwa kitendo alichokifanya huko Camp Nou juma lililopita.

Katika maelezo ya kutaka msamaha aliyoyatoa, baadhi ya vyombo vya habari vilimkariri tofauti na kudai kwamba meneja huyo kutoka nchini Ureno yu mbioni kutimka na kwenda kusaka maisha sehemu nyingine.

Endapo uchunguzi unaofanywa na shirikisho la soka nchini Hispania kufuatia sakata la Jose Mourinho la kumsukuma na kumfinya jicho meneja msaidizi wa FC Barcelona Tito Vilanova na ikathibitika alikua chanzo, kuna hatari ya kufungiwa michezo 12 itakayokua chini ya shirikisho hilo.

Katika hatua nyingine real Madrid wamefanikiwa kupata ushiundi wa mabao mawili kwa moja katika mchezo wa kirafiki uliokua na lengo la kuwania kombe la Santiago Bernabeu dhidi ya Galatasaray.

Selcuk Inan wa Galatasaray ndie alikua wa kwanza kupachika bao katika dakika ya kumi kabla ya beki wa pembeni wa The Galacticos Sergio Ramos kufunga bao la kusawazisha na Karim Benzema akipachika bao la pili na la ushindi.

No comments:

Post a Comment