KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 17, 2011

JOSE MOURINHO NA SAKATA LA WAANDISHI.

Meneja wa klabu ya Real Madrid Jose Mourinho, amerejea tena kitendo cha kuwakwepa waandishi wa habari, kama alivyofanya mwishoni mwa juma lililopita mara baada ya mchezo wa kwanza wa kuwania Spanish super Cup uliochezwa Estadio Stantiago Bernabeu.

Jose Mourinho amerejea kitendo hicho baada ya kumtuma kwa mara nyingine tena msaidizi wake Aitor Karanka, kuzungumza na vyombo vya habari kuhusiana na mchezo wa pili wa kuwanai Spanish Super Cup unaofanyika hii leo mjini Barcelona.

Katika mkutano wa mwishoni mwa juma lililopita, kitendo cha Jose Mourinho kutokuingia katika chumba cha waandishi wa habari kilichukuliwa kama hatua ya kuogopa kutoa maneno makali dhidi ya wapinzani wake ambao siku za nyuma alidai wanapendelewa wazi wazi na waamuzi.

Akizungumza katika mkutano huo Aitor Karanka, bado aliendelea kusisitiza jambo la kutekeleza majukumu kama utaratibu wa klabu unavyoagiza huku akiwataka waandishi wa habari kutoshtushwa na kitendo hicho cha Jose Mourinho kutojitokeza mbele yao.

Amesema wanakwenda katika mchezo wa hii leo, huku akiwamini watapata ushindi na kurejea mjini Madrid wakiwa na ubingwa wa Spanish Super Cup ambao kwa mara ya mwisho waliuchukuwa mwaka 2008.

Hata hivyo amedai kwamba endapo kiksoi chao kitacheza kama kilivyocheza katika mchezo wa mwanzo kutakuwa na uwezekano mkubwa wa kuwashinda kirahisi wapinzani wao ambao hii leo watakua nyumbani Camp Nou.

Katika hatua nyingine kiungo alierejea nyumbani Cesc Fabregas anatarajia kujumuishwa katika kikosi kitakachowavaa Real Madrid ambapo hata hivyo ataanzia benchi na kutoa nafasi kwa viungo wengine ili kuamsha upinzani.

Josep pep Guardiola Isala meneja wa Barcelona amesema kiungo huyo yupo tayari kwa ajili ya pambano la usiku huu na wala hana shaka nae zaidi ya kumtakia kila la kheri ili aweze kutimiza ndoto zake za kuichezea kwa mara ya kwanza klabu hiyo iliyomkuza.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Estadio Stantiago Bernabeu mwishoni mwa juma lililopita klabu hizo zilitoka sare ya mabao mawili kwa mawili.

No comments:

Post a Comment