KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 9, 2011

Kiiungo wa nchini Uholanzi Rafael van der Vaart amemtaka kiungo mwenzake kutoka nchini Croatia Luka Modric kusitisha mawazo ya kuihama Tottenham Hotspurs kwa sasa na badala yake kufikiria ni vipi ataisaidia klabu hiyo katika msimu mpya utakaoanza mwishoni mwa juma hili.

Rafael van der Vaart amemtaka Luca Modric kuwa katika hali hiyo kufuatia sakata la kutaka kusajiliwa na klabu ya Chelsea ambayo imeonyesha nia ya dhati ya kufanya hivyo kwa kuongeza kiasi cha pesa siku hadi siku.

Rafael van der Vaart amesema Luca Modric bado anahitajika katika kikosi cha Spurs kutokana na muhimili wake wa kiuchezaji uliowasaidia msimu uliopita ambao ulishuhudia wakicheza ligi ya mabingwa barani Ulaya na kufika kwenye hatua ya robo fainali.

Amesema licha ya kumtaka abaki kupitia vyombo vya habari, pia amekua na mawasiliano na kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, na kila leo anamuhusia jambo hilo ambalo ana hakika atalitimiza kwa kutoa maamuzi kabla ya kufungwa kwa usajili August 31 mwaka huu.

Wakati Rafael van der Vaart, akimuomba Luca Modric abaki huko White Hart Lane, uongozi wa Spurs tayari umeshaonyesha dalili za kumuachia kiungo huyo kufuatia taarifa zinazodai kwamba wanataka kumsajili kiungo kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Real Madrid Lassana Diarra.

Spurs wameripotiwa kuwa katika mazungumzo na viongozi wa Real Madrid na wakati wowote kuanzia hii leo huenda majibu kamili ya kuuzwa kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, yakaafikiwa na pande hizo mbili.

Lassana Diarra tayari alishawahi kucheza soka chini ya meneja wa Spurs Harry Redknapp, wakati akiwa na klabu ya Portsmouth mwaka mwaka 2008 na sasa anataka kumrejesha tena katika utawala wake.

Harry Redknapp pia anamuwinda kiungo kutoka nchini Uingereza na klabu ya West Ham Utd Scott Parker, lakini mawindo hayo yameingia dosari kutokana na mazungumzo binafsi kati ya mchezaji huyo wa uongozi wa Spurs kukwama, kwa madai ya kiungo huyo kuhitaji mshahara mkubwa kwa juma.

Spurs wana matumaini makubwa ya kukamilisha usajili wa wachezaji hao wawili endapo watafanikisha kuwauza wachezaji waliowaweka sokoni Jermaine Jenas pamoja na Wilson Palacios.

No comments:

Post a Comment