KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 4, 2011

King Kenny Dalglish ATAMBIA USAJILI WAKE.

Meneja wa majogoo wa jiji Liverpool King Kenny Dalglish amesema licha ya kufanya usajili wa wachezaji wanne mpaka sasa, bado ataendelea kufanya hivyo mpaka hapo atakapoona ameridhishwa na kile anachokifanya.

King Kenny Dalglish ametangaza dhamira hiyo katika hafla ya kuwatambulisha kwa waandishi wa habari wachezaji aliowasajili katika kipindi cha kuelekea msimu mpya wa ligi huku akitamba watamsaidia kwa kiasi kikubwa.

Amesema kila meneja wa klabu yoyote duniani, aliefanya usajili katika kipindi hiki anaamini alichokifanya ni sahihi, hivyo kwa upande wake hana shaka na mafanikio ya Liverpool katika msimu wa mwaka 2010-11.

Wachezaji walitambulishwa na King Kenny Dalglish katika hafla hiyo ni Jordan Henderson (Sunderland), Charlie Adam (Blackpool), Stewart Downing (Aston Villa) pamoja kipa Alexander Doni (AS Roma).

King Kenny Dalglish toka alipokabidhiwa madaraka la kukiongoza kikosi cha Liverpookl mwishoni mwa mwaka jana, tayari ameshatumia paund million 100, katika usajili wa wachezaji hatua ambayo inaungwa mkono na mmiliki wa klabu hiyo ya Meceyside John W Henry.

Wachezaji wengine ambao bado wapo katika rada ya meneja huyo kutoka nchini Scotland ni beki wa pembeni wa Newcastle Utd Jose Enrique , beki wa kati kati wa Bolton Wanderers Gary Cahill pamoja na beki mwingine wa Birmingham City Scott Dann.

Wakati huo huo nahodha na kiungo wa klabu ya Liverpool, Steven Gerrard ataendelea kuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja zaidi, kufuatia maumivu wa nyonga yanayomkabili kwa sasa.

Steven Gerrard, ambae alipewa nafasi ya kujumuika na wachezaji wengine huko Anfield mwanzoni mwa msimu ujao, ameongezea muda wa kuendelea kuuguza jeraha lake ambalo limeshindwa kupona kwa muda mufaka.

King Kenny Dalglish amezungumzia hatua hiyo katika mkutano na waandishi wa habari ambapoa mesema kuchelewa kwa mshambuliaji huyo bado hakumpi shida kutokana na kuwa na kikosi kizuri, lakini pia akamtakia kila la kheri ili aweze kurejea uwanjani akiwa na afya njema.

No comments:

Post a Comment