Kiungo Kwadwo Asamoah ameachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ghana kitakachocheza kesho.
Kwado ameondolewa kikosini kufuatia taarifa aliyoituma kutoka nchini Italia akiwa na klabu yake ya Udanise ambapo ameeleza kwamba amepatwa na maumivu wa kifundo cha mguu akiwa katika maandalizi ya msimu mpya wa ligi.
Hata hivyo wachezaji wengine walioitwa na kocha mkuu Goran Stevanovic kutoka nje ya bara la Afrika wameshawasili kambini na kesho wanatarajia kujumuyishwa kikosini.
Michezo mingine ya kimataifa ya kirafiki kwa bara la Afrika itachezwa siku ya jumatano ambapo;
Senegal v Morocco, Dakar
Africa Kusini v Burkina Faso - Johannesburg
Gabon v Guinea - Paris
Equatorial Guinea v Guinea-Bissau - Lisbon
Zimbabwe v Zambia - Harare
Tunisia v Mali - Monastir
Ivory Coast v Israel - Geneva
Botswana v Kenya - Gaborone
Liberia v Angola - Monrovia
Malta v jamuhuri ya Afrika ya kati - Malta
The Gambia v DR Congo - Banjul
No comments:
Post a Comment