KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 3, 2011

LAMPARD AJIBU TUHUMA ANAZOTUPIWA.

Kiungo wa klabu ya Chelsea, Frank Lampard amewapasha habari wale wanaombeza kwa kusema zama zake za kusakata soka zimekwisha kwa kuwaeleza kwamba yeye bado wamo katika medini ya soka na wala hadhani kama amefikia kiwango cha kushindwa kuonyesha uwezo anapokua uwanjani.

Frank Lampard ambae kwa sasa yu sanjari na kikosi cha Chelsea katika maandalizi ya msimu mpya wa ligi, amesema wanaombeza wamekua wakichukulia kigezo cha umri alio nao lakini kwake haoni sababu ya kuona umri unamzuia kucheza soka.

Amesema wapo wachezaji wenye umri mkubwa kama yeye huku akichukulia mfano wa winga wa Man utd Ryan Giggs ambae mpaka hii leo anacheza soka akiwa na umri wa miaka 37, sasa iweje afikiriwe yeye na si gwiji huyo wa old Trafford alihoji Lampard.

Lampard, mwenye umri wa miaka 33, amelazimika kulisema hiyo katika maadhimisho ya miaka kumi baada ya kuihama klabu yake ya zamani ya West ham Utd na kujiunga na Chelsea mwaka 2001 kwa ada ya uhamisho wa paund million 11.

Lampard ameahidi kufanya makubwa zaidi ya yale aliyoyaonyesha siku za nyuma hatua mbayo anaamini itawaziba midomo mahasimu wake wanaombeza kwa kigezo cha umri ambacho kwake amekitupilia mbali.

Hata hivyo kushuka kwa kiwango cha mchezaji huyo, kumechangiwa kwa kiasi iikubwa na majeraha yanayomkabili mara kwa mara na kufikia wakati kuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu, na gonjwa kubwa linalomsumbua ni kubanwa na ngiri kinapofika kipindi cha baridi huko barani Ulaya.

No comments:

Post a Comment