KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 23, 2011

LIVERPOOL KUMRUDIA Craig Bellamy.

Majogoo wa jiji Liverpool wameushtua ulimwengu wa soka kufuatia mipango yao ya kutaka kumrejesha kundini kiungo mshambuliaji kutoka nchini Wales na klabu ya Man City Craig Bellamy.

Liverpool wamepanga mipango hiyo kupitia ombi la meneja wao King Kenny Dalglish ambae bado amepania kukiboresha kikosi chake, ambacho mpaka sasa kimeshajikusanyia point nne katika msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Mipango ya Liverpool ya kutaka kumrejesha kundini Craig Bellamy, huenda ikafanikiwa kufuatia mchezaji huyo kuwekwa kando na meneja wa Man City Roberto Mancini na kufikia wakati kutokufanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha klabu hiyo ya Etihad Stadium.

Msimu uliopita Craig Bellamy, alipelekwa kwa mkopo Cardif City akitokea Man City baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza, lakini pia hatua hiyo ilichagizwa na malumbano kati yake na Roberto Mancini ambae alionyesha dhahiri kutokumuhitaji.

Wakati Liverpool wakijiandaa kutuma ofa ya kutaka kumsajili Bellemy tayari kuna baadhi ya klabu zimeshaonyesha nia kama hiyo ambazo ni Sunderland, Stoke City, Bolton na Everton zote za nchini Uingereza pamoja na Celtic ya nchini Scotland.

Craig Bellamy mwenye umri wa miaka 32, alipata nafasi ya kuitumikia Liverpool katika msimu wa mwaka 2006-07 ambapo alicheza michezo 27 na kufunga mabao saba.

No comments:

Post a Comment