KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 18, 2011

Luka Modric AENDELEA KUWAUMIZA VICHWA SPURS.

Meneja wa Tottenham Hotspurs Harry Redknapp anaamini endapo kiungo kutoka nchini Croatia Luka Modric atauzwa klabuni hapo ataweza kukamilisha mipango ya kuwasajili wachezaji wengine ambao watakiongezea nguvu kikosi chake.

Harry Redknapp, ambae alikua anapinga hatua ya kuuzwa kwa kiungo huyo anaewaniwa na klabu ya Chelsea ameonyesha kuwa tayari suala hilo, huku akimini kuruhusiwa kuondoka kwa Luka Modric bado hakutoathiri uwezo wa kikosi chake kitakapokua uwanjani.

Amesema mpaka sasa bado wana matumaini ya aina mbili ambapo tumaini la kwanza ni kuendelea kubaki na mchezaji huyo na kama itashindikana ni bora kuuzwa kwa ajili ya kumpa uhuru wa kutimiza malengo yake.

Hata hivyo Harry Redknapp, amemtetea mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy ambae anatuhumiwa kuwa kizingiti cha kutompa ruhusa Luca Modric kuondoka klabuni hapo baada ya kufanya nae mkutano mwezi uliopita.

Tottenham Hotspurs kwa sasa wanajipanga kufanya usajili wa kiungo kutoka nchini Uingereza pamoja na West Ham Utd Scot Parker, kiungo wa nchini Ufaransa na klabu ya real Madrid ya nchini Hispania Lassana Diarra pamoja na mshambuliaji kutoka nchini Togo na klabu ya Man City Emmanuel Adebayor.

Katika suala la kusajiliwa kwa Lassana Diarra tayari kuna dosari kufuatia uongozi wa Real Madrid kuikataa ofa iliyotumwa na Spurs juma lililopita huku ukidai haupo tayari kumuuza kiungo huyo mwenye umti wa miaka 24.

No comments:

Post a Comment