KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 19, 2011

MAN UTD NDANI YA WINGU ZITO LA MAJERUHI.

Beki kutoka nchini Serbia na klabu bingwa nchini Uingereza Man Utd Nemanja Vidic, atakua nje ya uwanja kwa kipindi cha majuma matano kufautia maumivu ya nyama za paja yanayomkabili toka mwishoni mwa juma lililopita.

Nemanja Vidic, alipatwa na maumivu hayo katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza mwishoni mwa juma lililopita ambapo Man Utd, walicheza na West Bromwich Albion na kufanikiwa kupata ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Meneja wa Man Utd Sir Alex Ferguson amesema, siku tatu zilizopita walidhani huenda Nemanja Vidic ingemchukua muda mchache kurejea uwanjani lakini majibu ya vipimo alivyofanyiwa, yamedhihirisha atakua nje kwa kipindi kirefu.

Ferguson pia akazungumzia upande wa Rio Ferdinand ambae nae hakumaliza katika mchezo wa ufunguzi wa ligi dhidi ya West Brom kwa kusema beki huyo hatotujumuishwa kikosini katika mpambano wa siku ya jumapili dhidi ya Tottenham Hotspurs kufuatia maumivu wa nyama za paja yanayomuandama kwa sasa.

Hata hivyo mzee huyi kutoka nchini Scotland amedai kwamba Ferdinand huenda akarejea mapema uwanjani, zaidi ya Nemanja Vidic kutokana na udogo wa jaraha lake ambapo anakadiriwa huenda akajumuishwa katika kikosi kitakachowavaa Arsenal mnamo August 28.

Kwa upande wa beki wa pembeni kutoka nchini Brazil Rafael Da Silva, amesema hatokuwepo uwanjani kwa kipindi cha majuma kumi, ambapo hatua hii inatokana na upasuaji wa bega aliofanyiwa na jopo la madaktari klabuni hapo.

Katika hatua nyingine Sir Alex Ferguson amekiri kuzipokea kwa furaha taarifa za kupona kwa beki wa pembeni kutoka nchini Ufaransa Patrice Evra ambae hakucheza katika mchezo uliopita ilihali mshambuliaji kutoka nchini Mexico Javier Hernandez Balcazer Chicharito akiwa katika hali nzuri pia.

No comments:

Post a Comment