KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 2, 2011

Manuel Neuer MCHEZAJI BORA UJERUMANI 2010-11.

Kipa alisajiliwa na mabingwa wa zamani wa soka nchini Ujerumani Bayern Munich Manuel Neuer, ametangazwa kuwa mchezaji bora wa msimu uliopita ambao ulishuhudia akiitumikia Schalke 04, iliyopata mafanikio ya kucheza hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulya.

Manuel Neuer, ametangazwa kinara wa nafasi hiyo kufuatia kuwaangusha wapinzani wake ambao ni mshambuliaji wa Bayern Munich Mario Gomez alieshika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na , kiungo mpya wa klabu ya Real Madrid Nuri Kâzım Şahin ambae msimu uliopita aliwatumikia mabingwa wa nchini Ujerumani Borussia Dortmund.

Kufuatia hatua hiyo Manuel Neuer anakua kipa wa kwanza kutangazwa kuwa mchezaji bora nchini Ujerumani baada ya miaka kumi kupita, ambapo kwa mara ya mwisho kipa alietwaa tuzo hiyo alikua Oliver Kahn mwaka 2001.

Akizungumza kwa furaha mara baada ya kukabidhiwa tuzo yake, Manuel Neuer alisema alipata mshutuko mkubwa kusikia jina lake likitajwa kuwa kinara wa mchuano huo ambapo aliamini huenda asiongefikia hapo alipo kutokana na wapinzani wake kufanya vyema msimu uliopita.

Wakati Manuel Neuer akitangazwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora kwa msimu wamwaka 2010-11, kikosi cha Bayern Munich usiku wa kuakia hii leo kilianza vyema safari ya kusaka ubingwa wa kombe la nchini Ujerumani msimu wa mwaka 2011-12 baada ya kuibanjua klabu inayoshiriki ligi daraja la pili nchini humo Eintracht Braunschweig mabao matatu kwa sifuri.

Mabao hayo ya ushindi yalipachikwa wavuni na washambuliaji Thomas Mueller, Mario Gomez pamoja na kiungo Bastian Schweinsteiger.

Meneja wa kikosi cha klabu hiyo ya Allianze Arena Jupp Heynckes, amesifia mafanikio hayo yaliyopatikana usiku wa kuamkia hii leo huku akieleza wazi kwamba wachezaji wake wameonyesha hali ya kujiamini, ishara ambayo anaichukulia kama mwanzo mzuri wa msimu.

Bayern Munich wamefanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo ya kombe la Ujerumani huku vigogo vingine kama Bayer Leverkusen, Wolfsburg, Werder Bremen pamoja na Freiburg vikitupwa nje katika michezo ya mwishoni mwa juma lililopita.

No comments:

Post a Comment