KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 3, 2011

Mauro Zarate KUIHAMA SS LAZIO.


Raisi wa Società Sportiva Lazio, *SS Lazio* Claudio Lotito amesema wapo tayari kumuuza mshambuliaji kutoka nchini Argentina pamoja na wa klabu hiyo ya mjini Roma Mauro Zarate kwa kiasi kikubwa cha fedha.

Claudio Lotito ametangaza dhamira hiyo kufautia klabu za nchini Uingereza Arsenal na Man City pamoja na klabu ya nchini Ufaransa Paris St Germain kupigana vikumbo katika harakati za kuiwania saini ya mshambuliaji huyo.

Amesema wameona ni bora kumuweka sokoni Mauro Zarate mwenye umri wa miaka 24, ili kumaliza zogo linalozungumzwa nje ya klabu yao, hatua ambayo wanaichukulia kama sehemu ya malumbano ili hali wanahitaji pesa zitakazotokana na usajili wake.

Hata hivyo raisi huyo wa SS Lazio, amedai kuwa mpaka sasa bado hawajapokea ofa yoyote kutoka kwenye klabu hizo tatu na ndio maana wamepata nafasi ya kujadili na kuona umuhimu wa kutangaza ofa ambayo bado hawajaiwekwa hadharani.

Mauro Zarate tayari ameshacheza soka nchini Uingereza akiwa na klabu ya Birmingham City, baada ya kusajiliwa kwa mkopo katika msimu wa mwaka 2008-09 na alifanikiwa kucheza michezo 14 na kupachika mabao 4.

No comments:

Post a Comment