KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 16, 2011

MABINGWA WA ITALIA WAMUWANIA Thiago Alcantara.

Mtendaji mkuu wa mabingwa wa soka nchini humo AC Milan Adriano Galliani amesema kwa sasa wapo katika mazungumzo na wakala wa kiungo kutoka nchini Hispania na FC Barcelona Thiago Alcantara kwa ajili ya kutafuta uwezekano wa kumsajili.

Adriano Galliani amesema wanatambua hatua hiyo itakua ngumu kufuatia uongozi wa Barcelona kumuhitaji kwa hali na mali Alcantara, lakini wanaamini mazungumzo yanaweza kuwa suluhisho la kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20.

Amesema wakala wa Alcantara, aitwae Giovanni Branchini tayari alishafanya mazungumzo na uongozi wa AC Milan na sasa amerejea tena kufanya hivyo huku akiahidi kutoa ushirikiano katika suala hilo.

Ac Milan wana matumaini ya kumsajili Thiago Alcantara, kufuatia kusajiliwa na aliekua nahodha na kiungo wa klabu ya Arsenal Cesc Fabregas anaepewa nafasi kubwa ya kuwa mrithi wa Xavi Harnandez ambae atafikisha umri wa miaka 32 mwezi Februari mwaka 2012.

Kabla ya kusajiliwa kwa Cesc Fabregas, Thiago Alcantara, alipewa nafasi kubwa ya kumrithi mkongwe huyo, lakini sasa nafasi inaonekana kuwa finyu, na tayari inaaminiwa kuwa, njia sahihi ya kujiokoa ni kuondoka klabuni hapo na kwenda kusaka mafanikio sehemu nyingine.

No comments:

Post a Comment