KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 26, 2011

Mesut Ozil KIKOSINI KWA MARA NYINGINE TENA.

Kiungo mchezeshaji wa klabu ya Real Madrid Mesut Ozil amerejeshwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani baada ya kuachwa kwenye kikosi kilichocheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi Brazil ambao walibamizwa mabao matatu kwa mawili.

Mesut Ozil amerejeshwa kikosini, huku kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew akitetea maamuzi yake ya kumuacha katika mchezo uliopita ambapo amesema alifanya hivyo kwa ajili ya kumpa nafasi ya kupumzika mara baada ya kumaliza ziara ya nje ya barani Ulaya akiwa na klabu ya Real Madrid ambayo ilikua inajiandaa kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22, anatarajiwa kuwepo katika mchezo wa kuwanai nafasi ya kufuzu kucheza fainali za mataifa ya barani ulaya dhidi ya Poland utakaopigwa mwanzoni mwa mwezi ujao.

Katika hatua nyingine kiungo Sami Khedira, anaeichezea Real Madrid ametemwa katika kikosi hicho kufuatia maumivu ya misuli yanayomkabili kwa sasa hali ambayo ilimsababishia kuukosa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Brazil mwanzoni mwa mwezi huu.

Nae Beki wa Werder Bremen Per Mertesacker amerejeshwa kikosini baada ya kucheza kwa mara ya mwisho akiwa na timu ya taifa mwezi March mwaka huu, kutokana na majeraha ya muda mrefu yaliyokua yakimkabili.

Kikosi kamili ha Ujerumani kilichoitwa na kocha Joachim Loew upande wa wa:

Makipa:
Manuel Neuer (Bayern Munich), Tim Wiese (Werder Bremen), Ron-Robert Zieler (Hannover);

Mabeki:
Holger Badstuber, Philipp Lahm, na Jerome Boateng (all Bayern Munich), Marcel Shimelzer, na Mats Hummels(all Borussia Dortmund), Benedikt Hoewedes (Schalke), Per Mertesacker (Werder Bremen), Christian Traesch (Wolfsburg);

Viungo:
Toni Kroos, Bastian Schweinsteiger, na Thomas Mueller (all Bayern Munich), Sven Bender, na Mario Goetze (all Borussia Dortmund), Simon Rolfes na Andre Shuerro (all Bayer Leverkusen), Mesut Ozil (Real Madrid), Lukas Podolski( FC Cologne), Marco Reus (Borussia Moenchengladbach);

Washambuliaji:
Mario Gomez (Bayern Munich) na Miroslav Klose (Lazio).

No comments:

Post a Comment