KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 2, 2011

MIMI NI SHABIKI NAMBA MOJA WA Wesley Sneijder - Paul Scholes.

Kiungo alietangaza kubwaga manyanga katika medini ya soka mwezi May mwaka huu, Paul Scholes, ameibuka na kumpigia chepuo kiungo wa kimataifa toka nchini Uholanzi Wesley Sneijder kwa kusema anastahili kuziba nafasi yake kwenye kikosi cha Manchester United.

Paul Scholes, ameibuka na suala hilo alipohojiwa katika moja ya vipindi vya televisheni ya klabu ya Man utd, ambapo amesema yeye binafsi anamkubali kiungo huyo kwa asilimia 100, na wala hatopinga endapo atasajiliwa na Sir Alex Ferguson.

Amesema kubwa linalotakiwa kwa sasa ndani ya kikosi cha Man Utd ni kutengenezwa kwa kikosi imara ambacho kitatetea taji la nchini Uingereza na pengine kufika katika hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya na kutwaa taji la michuano hiyo ambalo msimu uliopita walishindwa kulichukua katika ardhi ya nyumbani kufuatia kisago cha mabo matatu kwa moja walichokipokea toka kwa FC Barcelona.

Kiungo huyo alieitumikia Man Utd kwa kipindi cha miaka 12 mfululizo, ameongeza kwamba, Wesley Sneijder ana uzoefu wa muda mrefu na uchezaji wake hauna tofauti na ule wa kikosi cha Man utd, hivyo anaamini atakapowasili old Trafford hakuna kitakacho haribika.

Kama itakumbukwa vyema, hapo jana Wesley Sneijder alitamka kwa mdomo wake kwa kusema yu tayari kujiunga na Man utd endapo klabu hiyo kongwe nchini Uingereza itakua na nia thabit ya kutaka kumsajili.

Hata hivyo akadai kwamba kwa sasa bado anajitambua kama mchezaji halali wa Inter Milan na katu hawezi kujichanganya na maneno yanayozungumzwa dhidi yake ya kutaka kusajiliwa na Man Utd, hadi kufikia wakati akashindwa kujiandaa na msimu mpya wa ligi ya nchini Italia.

Man utd kupitia kwa mtendaji mkuu David Gill wameshathibitisha kuhitaji mchezaji mmoja anaecheza nafasi ya kuingo, lakini hata hivyo meneja Sir Alex Ferguson ameshafunga mjadala wa kumsajili Wesley Sneijder kwa kusema hana mpango wa kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment