KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 3, 2011

PELE AENDELEA KUMKANYA NAYMARGwiji wa soka ulimwenguni Edison Arantes do Nascimento Pele, ameendelea kumkanya, mshambuliaji kinda wa kibrazil Naymar Do Santos Junior, kufuatia sakata la kuhusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na vilabu vya soka Barani Ulaya.

Edison Arantes do Nascimento Pele, kwa siku kadhaa sasa amekua akimshauri Naymar kuwa mtulivu na kuendelea kuitumikia klabu yake ya sasa Santos Fc ya nchini Brazil na wala asipaparike na taarifa za kutaka safari ya kuanza maisha barani Ulaya.

Pele, amesema mshambuliaji huyo ambae kwa sasa ni gumzo duniani, ana uwezo mkubwa wa kucheza soka, akiwa nyumbani kwao Brazil na wala hana shaka na hilo, hivyo atamsikitikia endapo atafikia maamuzi ya kuondoka nyumbani.

Amesema hakuna mchezaji asietaka kucheza soka barani Ulaya kwa sasa kutokana na ushindani mkubwa uliopo sambamba na michuano mizuri yenye kuvutia, lakini kwa kijana mdogo kama Naymar mwenye umri wa miaka 19 anastahili kutuliza akili yake kwa ajili ya kujipanga na maisha ya baadae.

Alipoulizwa ni wapi angependa mshambuliaji huyo acheze soka lake endapo itatokea amefanya maamuzi ya kuelekea barani ulaya, Pele amesema atapendezwa sana kama atamuona Naymar akijiunga na klabu za nchini Uholanzi, Hispania pamoja na Ufaransa na si Uingereza na Italia kwa madai kwamba soka la nchi hizo mbili ni gumu kwa mchezaji mdogo kama yeye.

Mwanzoni mwa mwezi Juni mwaka huu Naymar Do Santos Junior, alizusha zogo kubwa kwa vilabu kama Real Madrid, Chelsea, Man Utd, Fc Barcelona pamoja na Inter Milan ambavyo vyote kwa pamoja vilipigana vikumbo kwa kutaka kumsajili.

Vioja hivyo vilifikia tamati baada ya raisi wa klabu ya Santos Luis Álvaro kufutilia mbali mipango ya kuuzwa kwa Naymar Do Santos Junior huko barani Ulaya.

No comments:

Post a Comment