KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 8, 2011

Per Mertesacker ANUKIA UINGEREZA.

Beki wa nchini humo Per Mertesacker anajiandaa kuihama Weder Bremen na pengine huenda akajiunga na klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza.

Per Mertesacker, ambae kwa muda mrefu amekua akihusishwa na taarifa za kutaka kuihama klabu hiyo, amekua na wakati mgumu wa kulazimishwa asaini mkataba mpya huko Weserstadion lakini yeye binafsi ameendelea na msimamo wa kutotaka kufanya hivyo.

Akihojiwa na gazeti la michezo nchini Ujerumani, beki huyo mwenye umri wa miaka 26, amesema ni faraja kubwa sana kukaribia kuondoka katika ardhi ya nchini nyumbani kwao kufuatia kuwa na hitaji la muda mrefu la kutaka kucheza soka nje ya nchi yake.

Per Mertesacker amdai kwamba kucheza soka la nje ya nchi Ujerumani kutamsaidia kukuza kiwango chake na pengine kutamfanya kucheza kwa kiwango cha juu atakapoitwa kwenye timu ya taifa ya Ujerumania ambayo imekua inashindwa kufikia malengo ya kutwaa vikombe vikubwa duniani.

Nae mkurugenzi wa michezo wa Weder Bremen Klaus Allofs amesema upande wao kama viongozi wameshindwa kuafikiana na Per Mertesacker, katika suala la kusaini mkataba mpya na jibu wanalolipata kutoka kwake ni kuhitaji kucheza soka nje ya la nchini Ujerumani.

Per Mertesacker, amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumukia Weder Bremen na endapo hatoauzwa katika kipindi hiki ama mwezi januari mwaka 2012, ataondoka klabuni hapo akiwa kama mchezoji huru mwishoni mwa msimu huu.

Wakati Arsenal wakihusishwa na taarifa za kutaka kumsajili Per Mertesacker, bado wanafikiria kumsajili mmoja kati ya mabeki hawa Gary Cahill wa Bolton Wanderers, Criss Samba wa Blackburn Rovers na Phil Jagielka wa Everton.

No comments:

Post a Comment