KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 10, 2011

Peter Crouch pamoja na kiungo Wilson Palacios WATAKIWA BRITANNIA STADIUM.

Mwenyekiti wa Stoke city Peter Coates amesema wametuma ofa kwa mara ya mwisho huko White Hart Lane kwa lengo la kutaka kumsajili mshambuliaji wa Spurs Peter Crouch pamoja na kiungo Wilson Palacios.

Peter Coates amesema wamelazimika kutuma ofa ya mwisho baada ya mazungumzo ya kutaka kuwasajili wachezaji hao kuvunjika siku za awali kwa kigezo cha madai ofa walizotuma zilikua hazilingani na uwezo wa mshambuliaji Peter Crouch pamoja na kiungo Wilson Palacios.

Amesema endapo ofa waliyoituma huko White Hart lane itashindikana wataachana na utaratibu wa kutaka kuwasajili wachezaji hao wawili na watahamishia mawazo yao kwa wachezaji wengine ambao watapendekezwa na na meneja wa kikosi chao Tonny Pulis.

Wakati Stoke City wakithibitisha kukamilisha utaratibu wa kutuma ofa yao ya mwisho, huko Ashburton Grove, kiungo kutoka nchini Urusi Andrei Arshavin amekanusha vikali taarifa za kuwa mbioni kurejea nyumbani kwao na kujiunga na klabu ya Anzhi Makachkala.

Andrei Arshavin, amekanusha taarifa hizo ikiwa imepita siku moja baada ya vyombo vya habari vya nchini Urusi kuliainisha jina lake kuwa la pili kusajiliwa na klabu hiyo ambayo tayari imekamilisha usajili wa Yuri Zhirkov akitokea Chelsea.

Pia klabu hiyo imepania kumsajili mshambuliaji wa kutoka nchini Cameroon na klabu bingwa duniani Inter Milan Samuel Eto'o.

Wakati Andrei Arshavin, akikanusha taarifa za kuondoka Arsenal, mshambuliaji wa klabu hiyo Nicolas Bendtner amesema wakati wowote kabla ya August 31 ataondoka Emirates Stadium na kujiunga na klabu ambayo hakuwa wazi kuitaja.

Amesema kila kitu kwa sasa kinakwenda vizuri na anaamini mipango inayoendelea kupangwa na wakala wake itakamilika na atafurahia uhamisho wake ambao utampa nafasi kucheza kila juma, kitu ambacho amekua akikihitaji kwa kipindi kirefu.

No comments:

Post a Comment