KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 18, 2011

Petr Cech KUKOSA MCHEZO WA JUMAMOSI.


Kipa kutoka jamuhuri ya Czech pamoja na klabu ya Chelsea Petr Cech atakua nje ya uwanja kwa kipindi cha majuma matatu hadi manne kufuatia maumivu ya goti yanayomkabili kwa sasa.

Meneja wa klabu ya chelsea, Andre Villas-Boas imeeleza kuwa Petr Cech amepatwa na maumivu makali ya goti akiwa katika mazoezi ya kujaindaa na mchezo wa mwishoni mwa juma hili ambapo chelsea watawakaruibisha nyumbani West Brom katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza iliyoanza mwishoni mwa juma lililoputa.

Andre Villas-Boas amesema mara baada ya kupatwa na maumivu hayo Petr Cech, alianza kufanyiwa matibabu akiwa katika uwanja wa mazoezi na kisha alikwenda kufanyiwa vipimo na ikafahamika ameumia kwa kiasi kikubwa.

Amesema ni pigo kubwa sana kwake, kuumia kwa kipa huyo hasa ikizingatiwa amekuwa mchezaji tegemezi katika kikosi cha kwanza, cha The Blues ambacho mwishoni mwa juma lililopita kililazimishwa sare ya bila kufungana dhidi ya Stoke city.

Kwa mantiki hiyo sasa kipa huyo mwenye umri wa miaka 29 ataikosa michezo mingine ya ligi dhidi ya Norwich City pamoja na Sunderland huku akipewa nafasi ya kurejea tena uwanjani Septemba 18 katika mchezo utakaoshuhudia Chelsea wakipambana na Man utd.

Kuumiwa kwa Petr Cech, kunatoa nafasi kwa kipa chaguo la pili Henrique Hilario kuchukua nafasi katika kikosi cha kwanza.

No comments:

Post a Comment