KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 9, 2011

REAL MADRID WAANDIKA HISTORIA KATIKA USAJILI.Wafalme wa soka wa mji wa Madrid, Real Madrid wameandika historia baada ya kufanikisha usajili wa mototo mwenye umri wa miaka saba kutoka nchini Argentina aitwae Leonel Angel Coira.

Wafalme hao wa soka wa mji wa Madrid wamekamilisha azma hiyo baada ya kumfuatilia mototo huyo kwa kipindi kirefu kilichopita na kubaini ana kipaji cha hali ya juu ambacho kitawasaidia katika siku za usoni.

Msemaji wa Real Madrid Juan Tapiador, amesema Leonel Angel Coira bado ni mwanafunzi wa shule moja huko nchini Argentina lakini tayari wameshaafikiana na wazazi wake juu ya uhamisho wa kumpeleka mjini Madrid kwa ajili ya kuendelea na elimu sambamba na kuendeleza kipaji chake katika shule ya soka ya The Galacticos.

Amesema September 6 mwaka huu, Leonel Angel Coira ataongozana na wazazi wake hadi mjini Madrid kwa ajili ya kukamilisha masuala ya usajili wake pamoja na masuala mengine ambayo yatamnufainisha akiwa mjini Madrid akiendelezwa kiuchezaji.

Leonel Angel Coira pia alikua anawindwa vikali na mahasimu wa kubwa wa Real Madrid, Atletico Madrid.

No comments:

Post a Comment