KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 10, 2011

REAL MADRID WAIKATAA OFA YA SPURS.


Wafalme wa soka wa mjini Madrid, Real Madrid wameikataa ofa iliyotumwa huko Estadio Stantiago Bernabeu na uongozi wa Tottenham Hotspur kwa lengo la kutaka kumsajili kiungo kutoka nchini Ufaransa Lassana Diarra.

Real Madrid wameikataa ofa hiyo ambayo ilitumwa mwishoni mwa juma lililopita ambapo Spurs walidhamiria kumsajili Lassana Diarra kwa ada ya uhamisho wa euro Milion 18 (£15.8m) baada ya kukutana na kujadili kwa undani huku wakihitaji ushauri kutoka kwa meneja Jose Mourinho.

Katiika majadilino hayo meneja Jose Mourinho amesema hayupo tayari kumuuza kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 kutokana na mipango yake kumuhitaji kwa asilimia mia moja katika kikosi cha Real Madrid ambacho msimu ujao kimedhamiria kurejesha heshima iliyopotea kwa miaka minne sasa.

Meneja wa Spurs Harry Redknapp alitamani kumrejesha Lassana Diarra katika himaya yake baada ya kumuongoza alipokua Portsmouth, mwaka 2008 kabla ya kumuuza huko Estadio Stantiago Bernabeu mwaka 2009.

Sababu kubwa ya Diarra kuhitajika huko White Hart Lane, ni sakata linaendelea kwa sasa la kutaka kuondoka kwa kiungo kutoka nchini Croatia Luka Modric ambae anawaniwa na vilabu vya Manchester City pamoja na Chelsea.

No comments:

Post a Comment