KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 11, 2011

Richard Scudamore ATHIBITISHA MCHEZO MMOJA KUAHIRISHWA.


Chama cha soka nchini Uingereza kimetangaza kuuahirisha mchezo mmoja wa ligi kuu ya soka nchini humo itakayoanza mwishoni mwa juma hili kufautia vurugu zilizojitokeza jijini London kuanzai mwishoni mwa juma lililopita.

FA wamesema mchezo huo ambao hautochezwa ni ule uliopangwa kufanyika White Hart Lane kati ya wenyeji Tottenham Hotspurs dhidi ya Everton kutoka huko Goodson Park jijini Liverpool.

Mtendaji mkuu wa masuala ya ligi hiyo Richard Scudamore amesema wamelazimika kuuahirisha mchezo huo kufuatia mazingira ya mitaa ya Tottenham kutokua na usalama wa kutosha ambapo baadhi ya wananchi wanaopingana na jeshi la polisi wamevunja sehemu ya vioo vya uwanja wa White Haert Lane.

Richard Scudamore amesema pamoja na kufanya maamuzi hayo, hali ya sehemu ya mitaa ya Tottenham kwa sasa ipo shwari kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na jeshi la polisi, lakini ushauri walioupokea unawaelekeza kuusogeza mbele mchezo huo kwa ajili ya kuhofia vurugu ambazo huenda zikajitokeza tena.

Hata hivyo Richard Scudamore amesema licha ya kutoa utaratibu huo bado wataendelea kufanya mawasiliano na klabu zote zitakazoshiriki ligi kuu msimu wa mwaka 2011-12 kwa ajili ya kufahamu maendeleo ya kile kinachoendelea hadi hapo siku ya jumamosi ambapo wanaamini kila jambo litakua sawa.

Nahodha msaidizi pamoja na beki wa Spurs Michael Dowson, amesema kuahirishwa kwa mchezo wao wa ufunguzi imewauma lakini hakuna budi ya kukubaliana na hali halisi iliopo sasa katika mitaa ya klabu yao.

Amesema licha ya kuwa katika hali ya simanzi bado anaamini msimu wa mwaka 2011-12 utakua mzuri kwao na watafanya vyema na kufikia mafanikio ya kupata nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya kama ilivyokua msimu uliopita.

Michezo ya ligi kuu ambayo itaendelea kama ilivyokua imepangwa ni:

Blackburn - Wolverhampton

Fulham - Aston Villa

Liverpool - Sunderland

Queens Park Rangers - Bolton

Wigan - Norwich


Newcastle - Arsenal


JUMAPILI

Stoke - Chelsea

West Bromwich - Manchester United

No comments:

Post a Comment