KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 19, 2011

Ron-Robert Zieler AJUMUISHWA KIKOSINI.

Kipa wa klabu ya Hanover 96 Ron-Robert Zieler ameitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo ambacho kitaendelea na mpango wa kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Ulaya mapema mwezi ujao.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 22, ametajwa na kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Löw, akiwa kama chaguo la tatu, kufuatia kipa mwenye nafasi hiyo anaeitumikia klabu ya Bayer Leverkusen René Adler kufanyiwa upasuaji.

Hata hivyo bado kipa huyo aliewahi kusajiliwa na Man utd kuanzia mwaka 2005–2008 anapewa nafasi ya kubwa ya kuchezeshwa kati ya michezo miwili ya timu ya taifa ya Ujerumani, ambapo mchezo wa kwanza utakua Septemba 2 dhidi ya Austria na kisha utafuata mchezo wa kirafiki dhidi ya Poland mnamo septemba 6.

Joachim Löw amesema kuitwa kwa kipa huyo kunatokana na uwezo wake kupanda siku hadi siku na anaamini kutampa changamoto ya kujifunza mambo mengi ambayo atahitaji kuyafanyia kazi siku za usoni atakapoitwa kikosini akiwa kama chaguo la kwanza.

Timu ya taifa ya Ujerumani iliyo katika kundi la kwanza la michezo ya kuwnia nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya bara la Ulaya za mwaka 2012, inaongoza kundi hilo kwa kuwa na point 21, baada ya kuchomoza na ushindi katika michezo saba iliyopita ya kundi hilo.

No comments:

Post a Comment