KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 10, 2011

Rudi Voller AWAPASHA HABARI MASHABIKI.


Mkurugenzi wa michezo wa Bayer Leverkusen Rudi Voller ameyapa kisogo malalamiko ya mashabiki wa klabu hiyo ambao wanaonyesha kuchukizwa na hatua ya kikosi chao kuanza vibaya msimu wa mwaka 2011-12.

Rudi Voller ameyapa kisogo malalamiko hayo, kwa kusema katu hawawezi kufanya kazi kwa matakwa ya mashabiki ambao wameonyesha kumchukia meneja mpya wa Bayer Leverkusen Robin Dutt ambae ameshindwa kukiongoza kikosi chake kusonga mbele kwenye michuano ya kombe la nchini Ujerumani pamoja na kupoteza point tatu za mchezo wa ufunguzi wa ligi dhidi ya klabu ya Mainz.

Rudi Voller ambae aliwahi kuitumikia timu ya taifa ya Ujerumani pamoja na klabu za Kickers Offenbach , 1860 Munich , Werder Bremen, AS Roma , Olympique de Marseille pamoja na Bayer Leverkusen amesema kila shabiki huko BayArena anastahili kutambua kwamba meneja aliopo sasa klabuni hapo bado anahitaji muda wa kutosha wa kuendelea kupanga kikosi chake.

Amesema kuanza vibaya kwa kufungwa michezo miwiwli hakumaanishi watakua na msimu mbaya na yeye binafsi anaamini kila jambo litakwenda vyema siku za usoni na kila shabiki atafurahishwa na mtiririko wa ushindi utakaopatikana.

Bayer Leverkusen waliondoshwa kwenye michuano ya kombe la nchini Ujerumani July 30 baada ya kukubali kisago cha mabao manne kwa matatu kutoka kwa Dynamo Dresden, na katika mchezo wa ufunguzi wa ligi klabu hiyo ya Bay Arena, ilichapwa mabao mawili kwa sifuri na Mainz.

No comments:

Post a Comment