KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 16, 2011

SAKATA LA UHAMISHO LA RAUL.

Meneja wa Schalke 04, Ralf Rangnick ameendelea kukanusha uvumi unaomuhusu mshambuliaji wa klabu hiyo kutoka nchini Hispania Raul Gonzales Blanco wa kutaka kuondoka katika kipindi hiki.

Ralf Rangnick, amekanusha kwa mara nyingine taarifa hizo ambazo kwa sasa zinamuhusha Raul kutaka kujiunga na klabu ya Blackburn Rovers ya nchini Uingereza ambayo imeanza vibaya michezo ya ligi kufautia kukubalia kisago cha mabao mawili kwa moja kutoka kwa Wolveshampton Wandrerers.

Meneja huyo amesema taarifa hizo za mshambuliaji wake kutakiwa nchini Uingereza sio rasmi na wala hataki kuzipa nafasi kichwani mwake zaidi ya kuamini Raul Gonzales ataendelea kusalia katika himaya yake kama mkataba unavyomuamuru.

Hata hivyo Ralf Rangnick, ametanabai kuwa licha ya habari hizo kuzungumzwa na vyombo vya huko nchini Uingereza, mpaka sasa hawajapokea ofa yoyote kutoka Blackburn Rovers, hatua ambayo inaendelea kujidhihirisha ni uongo mtupu.

Hii si mara ya kwanza kwa Raul kuhusishwa na taarifa za kutaka kuihama Schalke 04, kwani mwanzoni mwa mwaka huu mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34 alihusishwa na taarifa za kutaka kujiunga na klabu ya Bazasport ya nchini Uturuki.

Na kwa mara ya pili alihusishwa na taarifa za kutaka kurejea nyumbani kwao Hispania kujiunga na klabu ya Malaga ambayo imepania kufanya mapinduzi ya soka msimu huu, lakini bado taarifa hizo hazikua na ukweli wowote.

Raul Gonzaleas alisajiliwa na Schalke 04, mwaka 2010 akitokea kwenye klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania ambayo alidumu nayo kwa kipindi cha miaka 14 na hii ilikua ni kuanzia mwaka 1994-2010.

No comments:

Post a Comment