KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 15, 2011

SAKATA ZITO KUIDHURU ARSENAL?

Kiungo wa klabu ya Arsenal Alexander Song Belong, huenda akaadhibiwa na chama cha soka nchini uingereza kufuatia kosa la kumkanyaga kwa makusudi kiungo wa Newcastle Utd Joel Barton wakati mchezo wa ufunguzi wa ligi uliochezwa St James Park.

Alexander Song Belong ameingia matatizoni baada ya kuthibika alifanya kitendo cha kumkanyaga Barton kwa makusudi, hatua Ambayo ilitafsiriwa kama sehemu ya kulipa kisasi cha kiungo huyo aliesababisha Gervinho kutolewa nje ya uwanja kwa kuonyesha kadi nyekundu.

Tayari muamuzi Peter Walton ameshawasilisha ripoti ya mchezo huo uliochezwa siku ya jumamosi na tukio hilo limejumuishwa na sasa inasubiriwa hukumu kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka.

Muamuzi wa zamani wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza, Dermot Garragher amesema kosa alilofanya Alexander Song Belong huenda likamgharimu kwa kufungiwa michezo zaidi ya miwili, lakini pia akayapinga maamuzi ya muamuzi wa mchezo huo kwa kusena Joel Barton alistahili kuonyeshwa kadi nyekundu kama ilivyokua kwa Gervinho.

Endapo adhabu hiyo itamkabili Alexander Song Belong, Arsenal itakua katika shaka kubwa la kujaza nafasi ya viungo katika mchezo wao unaofuata dhidi ya Liverpool, ambapo kama inavyofahamika Cesc Fabregas ametimkia Barcelona huku Jack Wilshire akiendelea kuuguza jeraha linalomkabili.

Meneja wa klabu ya Arsenal Arsène Wenger anafikiria kukata rufaa juu ya adhabu ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa Gervinho katika mchezo wa siku ya jumamosi dhidi ya Newcastle Utd.

Arsene Wenger amethibitisha taarifa za kufikiria kufanya hivyo akiwa katika mkutano na waandishi wa habari uliolenga kuzungumzoa mchezo wa kesho wa hatua ya mtoano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya klabu ya Udinense ya nchini Italia.

Gervinho alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumpiga usoni Joel Berton.

No comments:

Post a Comment