KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 12, 2011

SAMIR NASRI AENDELEA KUMTOA UDENDA MANCINI.Meneja wa Man city Roberto Mancini anaonyesha shauku ya kutaka kumsajili kiungo Samir Nasri huku akimini uongozi wa klabu hiyo utakamilisha masuala yote ya kumuhamisha kutoka jijini London hadi mjini Manchester siku za hivi karibuni.

Mancini amesema kikosi chake kwa sasa bado kinahitaji kuongezewa nguvu kwa wachezaji aliowapendekeza ili aweze kutimiza azma ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini Uiungereza msimu wa mwaka 2011-12.

Amesema suala la kusajiliwa kwa Samir Nasri anaimani litakamilishwa kwa wakati, lakini akakiri sio rahisi kama wengi wanavyofikiri.

Roberto Mancini pia akazungumzia suala la mshambuliaji kutoka nchini Argentina Carlos Tevez alieshupalia kuondoka klabuni hapo kutokana na kutopendezwa na mazingira ya mji wa Manchester, kwa kisingizio cha kutaka kuwa karibu na familia yake iliyo nyumbani kwao.

Mancini amesema suala la uhamisho wa mshambuliaji huyo bado halijakaa sawa lakini endapo atahitaji kubaki yeye kama meneja hatokua na tatizo lolote, ila anachofahamu Carlos Tevez anahitaji kuondoka Etihad Stadium.

Wakati huo huo meneja huyo kutoka nchini Italia akawashukuru mashabiki wa soka wa klabu ya Man city kwa utulivu waliouonyesha, kufuatai sakata la Carlos tevez la kutaka kuondoka.

No comments:

Post a Comment