KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 19, 2011

Samir Nasri NDANI YA KIKOSI CHA ARSENAL KITAKACHOWAVAA LIVERPOOL.


Kiungo kutoka nchini Ufaransa Samir Nasri, amejumuishwa katika kikosi cha Arsenal kitakachoshuka dimbani hapo kesho kuwakabili majogoo wa jiji Liverpool katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza iliyoanza mwishoni mwa juma lililopita.

Samir Nasri amejumuishwa kikosini na meneja Arsene Wenger huku akiwa anakabiliwa na taarifa za kutaka kuihama Arsenal na kuelekea Etihad Stadium yalipo makao makuu ya Man City kwa ada ya uhamisho wa paund million 22.

Arsene Wenger amethibitisha uwepo wa kiungo huyo katika mchezo wa kesho utakaochezwa Emirates Stadium, akiwa katika mkutano na waandishi wa habari uliokua unazunguzmoa mpambano huo utakaochezwa mishale ya saa nane mchana kwa saa hapa nyumbani.

Katika michezo miwili iliyopita ambayo Arsenal wameshacheza toka msimu huu ulipoanza ambapo katika mchezo wa kwanza The Gunners walicheza na Newcastle Utd na kupata matokeo ya sare ya bila kufungana na kisha mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Udanise waliolala bao moja kwa sifuri, Samir Nasri aliachwa nje ya kikosi.

Arsenal hiyo kesho watashuka ndimbini huku wakiwa na upungufu wa wachezaji waliozoeleka kucheza nafasi ya kiungo ambapo watamkosa Tomas Rosicky, Jack Wilshere na Abou Diaby ambao ni majeruhi huku Alex Song akiaanza kutumikia adhabu ya kufungiwa michezo mitatu na FA sambamba na mshambuliaji kutoka nchini Ivory Coast Gervinho.

Wakati huo huo meneja wa Man City Roberto Mancini, bado anaonyesha matumaini ya kutaka kumsajili kiungo Samir Nasri ambae amegoma kusaini mkataba mpya na klabu yake ya Arsenal huku mkataba uliopo sasa ukitarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Roberto Mancini, amesema katika siku 11 zilizosalia kabl ya dirisha la usajili halijafungwa anaamini kila kitu kitakua vizuri na watafikia malengo waliyojiwekea katika usajili wa mchezaji huyo.

No comments:

Post a Comment