KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 11, 2011

Samuel Eto'o KUANDIKA HISTORIA?


Mshambuliaji kutoka nchini Cameroon Samuel Eto'o huenda akaandika histori ya kuwa mchezaji atakaelipwa mshahara mkubwa barani Ulaya endapo atasajiliwa na klabu iliyopania kufanya mapinduzi ya soka la nchini Urusi Anzhi Makhachkala.

Samuel Eto'o anafikiriwa kuingia katika utaratibu huo kufautia uongozi wa klabu ya Anzhi Makhachkala kuonyesha kuwa tayari kumsajili katika kipindi hiki akitokea kunako klabu yake ya Inter Milan ya nchini Italia.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, ameripotiwa kuwa endapo atasajiliwa na klabu hiyo inayomilikiwa na mfanyabiashara wa mafuta, atalipwa kiasi cha paund laki tatu kwa juma ambao utamfanya kuwa juu zaidi ya wachezaji wengine ulimwenguni kote.

Kwa hivi sasa wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa kwa juma ni kiungo wa nchini Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi pamoja na kiungo kutoka nchini Ureno klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo.

Hata hivyo safari ya mshambuliaji huyo ambae msimu uliopita alifanikiwa kupachika mabao 34 akiwa na Inter Milan, imeshaanza kuonyesha dalili zote, kufuatia mtendaji mkuu The Nerrazuri Ernesto Paolillo kueleza kwamba kila kitu kwa hivi sasa kinakwenda vizuri.

Ernesto Paolillo ameliambia gazeti moja la michezo la nchini Italia kwamba mshambuliahi huyo anakaribia kujiunga na Anzhi Makhachkala kwa ada ya uhamisho wa Euro million 69.

Endapo Samuel Eto’o atafanikisha usajili huo, Inter Milan wanapewa nafasi ya kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Argentina na klabu ya Manchester City Carlos Tevez.

No comments:

Post a Comment