KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 29, 2011

Sergio Aguero AMBEMBELEZA TEVEZ KUBAKI MAN CITY.

Mshambuliaji mpya wa Man City Sergio Aguero amesema ana matumaini makubwa ya kumuona mshambuliaji mwenzake Carlos Tevez akisalia klabuni hapo licha ya kuhusishwa na taarifa za kutaka kuondoka katika kipindi hiki cha usajili.

Sergio Aguero ambae tayari ameshaifungia Man city mabao matatu toka alipoanza kuitumikia klabu hiyo mwanzoni mwa msimu huu, amezungumzia matumaini hayo ikiwa ni saa chache mara baada ya mpambano wa jana ambao ulishuhudia vijana wa Roberto Mancini wakiibuka na ushindi wa mabao matano kwa moja dhidi ya Spurs.

Amesema amezungumza na Carlos Tevez juu ya suala hilo na amemsihi asiondoke na kikubwa alichokiona ni matumaini kutoka kwa mshambuliaji huyo ambae alihitaji kurejea nyumbani kwao Argentina kwa dhumuni la kuwa karibu na familia yake yenye watoto wawili wa kike.

Sergio Aguero, ameongeza kwamba endapo Carlos Teves atabaki klabuni hapo hali ya ushindani katika kikosi cha Man City itaongezeka maradufu kutokana na ushupavu wa wachezaji waliopo ambao tayari wameshajiwekea matumaini ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Mwezi uliopita Carlos Tevez alikaribia kuondoka Etihad Stadium na kujiunga na Club Corinthians Paulista ya nchini Brazil lakini taratibu za uhamisho hazikuwahi muda kama ilivyokua imepangwa na pande hizo mbili.

Hata hivyo mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, bado anahusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na klabu bingwa duniani Inter Milan, ambayo imekubalia kumuachia mshambuliaji kutoka nchini Cameroon Samuel Eto’o ambae amejiunga na Anzhi Makashkhala ya nchini urusi.

Wakati huo huo.


Mshambulaiji kutoka nchini Paraguay Roque Santa Cruz amekamilisha mipango ya kujiunga na klabu ya Real Betis ya nchini Hispania akitokea Man City kwa mkopo wa muda mrefu.

Real Betis wamekamilisha usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, huku wakiamini atawasaidia katika harakati za kusaka ubingwa wa nchini Hispania msimu huu.

Roque Santa Cruz alipata mazingira magumu ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Man city, baada ya kuwa chini ya utawala wa mtaliano Roberto Mancini ambae alichukua nafasi ya Mark Hughes aliemsajili mshambuliaji huyo mwaka 2009 akitokea Blackburn Rovers.

Mwezi januari msimu uliopita Roque Santa Cruz, alirejeshwa kwa mkopo Blackburn Rovers kufuatia kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Man City.

No comments:

Post a Comment