KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 23, 2011

Sir Alex Ferguson AJITAMBIA VIJANA WAKE.


Meneja wa klabu bingwa nchini Uingereza Man Utd Sir Alex Ferguson, amekimwagia sifa kikosi chake kilichosheheni wachezaji chipukizi ambacho usiku wa kuamkia hii leo kilitembeza bakora dhidi ya Tottenham Hotspurs katika muendelezo wa michezo ya ligi nchini humo.

Sir Alex Ferguson amesema kwa hakika kikosi hicho kilionyesha mchezo mzuri na wenye kuvutia huku kila mchezaji aliempa nafasi ya kucheza akionyesha njaa ya kusaka ushindi ambao ulikua ni muhimu sana kwao.

Amesema kimtazamo mashabiki wengi walidhani huenda kikosi hicho kisingeweza kuonyesha upinzani dhidi ya Spurs ambao waliwatumia wachezaji wenye uzoefu kwa asilimia kubwa lakini, kujituma kwao kulimpa nafasi kila mmoja anaeishabikia Man utd kuamini kikosi hicho cha vijana kilihitaji ushindi.

Hata hivyo meneja huyo amedai kwamba, kipindi cha kwanza mpambano ulikua mgumu kwa kila upande na ilimlazimu kubadilisha mbinu katika kipindi cha pili ambacho kilishuhudia wakipata mabao matatu yaliyofungwa na Danny Welbeck, Anderson pamoja na Wayne Rooney.

Danny Welbeck, mwenye umri wa miaka 23 na siku 191 alipata nafasi ya kuzungumza na vyombo vya habari mara baada ya mtanange huo uliopigwa Old Trafford na kuelezea furaha yake ya kuifungia Man utd bao la kwanza katika mchezo wa ligi, baada ya kutolewa kwa mkopo msimu uliopita huko Stadium Of Light yalipo makao makuu ya Sunderland.

Kwa matokeo hayo sasa man Utd wanafikisha point sita baada ya kushuka dimbani mara mbili, na wanakamata nafasi ya pili wakiwa nyuma ya Man city ambao wanashikilia usukani kutokana na tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

No comments:

Post a Comment