KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 11, 2011

SOKA LA KENYA HUENDA LIKAINGIA PABAYA.


Waziri wa michezo nchini Kenya Paul Otuoma, ametoa angalizo kwa shirikisho la soka nchini humo KFF kuhakikisha uchaguzi mkuu wa viongozi unafanyika kabla ya Sepetember kumi mwaka huu.

Paul Otuoma ametoa angalizo hilo huku akisema endapo kamati ya uchaguzi itakaidi maagizo hayo, KFF itakua chini ya serikali ya jamuhuri ya nchi hiyo ambayo ipo chini ya raisi Mwai Kibaki.

Amesema anatambua maamuzi hayo yanaweza kuiweka pabaya nchi ya Kenya kufuatai kanuni na taratibu ya shirikisho la soka ulimwemnguni kote FIFA ambazo haziruhusu serikali kuingilia masuala ya soka.

Paul Otuoma amedai kwamba wamechoshwa na zogo linaloendelea ndani ya mchezo wa soka nchini humo na wao kama serikali wanaona njia rahisi ya kumaliza zogo hilo ni kufanyika kwa uchaguzi haraka iwezekanavyo ili kutoa nafasi kwa mambo mengine yanayohusu soka.

Amesema wao kama serikali wanatambua uwepo wa kamati ya uchaguzi iiliyoteuliwa na FIFA, lakini wanashangazwa na hatua ya kusita kwa kamati hiyo kuendelea na majukumu ya kumaliza sakata la uchaguzi ambao utawawezesha kupata viongozi wapya.

Hata hivyo taarifa zilizopo zinadai kwamba kamati ya uchaguzi wa FIFA imekua ikisigana na kamati ya uchaguzi wa shirikisho la soka nchini Kenya kwa madai ya kutotoa ushirikiano wa kutosha.

Sehemu ya ushirikiano ambayo imekwama ni kushindwa kuidhinishwa kwa fungu la fedha litakalowezesha kufanyika kwa uchaguzi huo, kutokupatikana kwa orodha ya wagombea pamoja na wapiga kura wanaostahili.

No comments:

Post a Comment