KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 9, 2011

Steven Pienaar NJE MIEZI MIWILI NA NUSU.


Kiungo wa nchini Afrika kusini na klabu ya Tottenham Hotspur Steven Pienaar atakua nje ya uwnaja kwa kipindi cha majuma sita yajayo kufuatia maumivu ya nyonga yanayomkabili kwa sasa.

Steven Pienaar amekumbwa na matatizo hayo akiwa na kikosi cha klabu yake ambacho mwishoni mwa juma lililopita kilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya Athletic Bilbao ya nchini Hispania.

Kiungo huyo ambae msimu uliopita aliitumikia Spurs katika michezo 11, alicheza mchezo huo wa kirafiki katika kipindi cha kwanza na alishindwa kuendelea katika kipindi cha pili kutokana na maumivu makali yaliyokua yakimuandama.

Kwa mantiki hiyo sasa Steven Pienaar mwenye umri wa miaka 29 hatokuwepo kwenye kikosi cha Spurs ambacho mwishoni mwa juma hili kitacheza mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya Everton.

No comments:

Post a Comment