KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 5, 2011

Thiago Alcantara KUWAVAA HISPANIA.


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo Vicente del Bosque amewashangaza wengi baada ya kumjumuisha kiungo chipukizi wa mabingwa wa soka barani Ulya Fc Barcelona Thiago Alcantara katika kikosi chake cha wachezaji 22 kitakachocheza mchezo wa kujipima nguvu juma lijalo dhidi ya timu ya taifa ya Italia.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20, amejumuishwa kikosini kufuatia uwezo wake mkubwa aliouonyesha akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ambacho kilifanikiwa kutwaa ubingwa wa barani Ulaya mwezi uliopita.

Vicente del Bosque ametoa sababu nyingine ya kumuita Thiago Alcantara, ambapoa mesema anataka kumpa uzoefu wa kutosha kwa ajili ya kutengeneza mazingira ya baadae ya nchi ya Hispania kwenye medani ya soka.

Thiago Alcantara, kabla ya kuichezea timu ya taifa ya vijana ya Hispania alikua na wakati mgumu wa kufanya maamuzi ya wapi acheze soka lake la kimataifa kufuatia kuwa na uraia wa nchini Brazil, ulisababishwa na baba yake mzazi Mazinho ambae alikua miongoni mwa wachezaji walioiwezesha Brazil kutwaa ubingwa wa dunia mwaka 1994 kule nchini Marekani.

Wachezaji walioachwa katika kikosi cha nchini Hispania ambacho kitacheza na Italia juma lijalo ni beki na nahodha msaidizi Carles Puyol, Joan Capdevila pamoja na Cesc Fabregas ambapo wote kwa sasa wanaendelea kurejesha hali zao za kawaida wakiwa na vikosi vya klabu zao kufuatia majeraha yaliyokua yakiwaandama.

Kikosi kamili kilichotajwa na Vicente del Bosque kwa upande wa;

Makipa: Iker Casillas (Real Madrid), Victor Valdes (Barcelona), Pepe Reina (Liverpool).

Mabeki: Alvaro Arbeloa (Real Madrid), Sergio Ramos (Real Madrid), Raul Albiol (Real Madrid), Gerard Pique (Barcelona), Andoni Iraola (Athletic Bilbao).

Viungo: Xabi Alonso (Real Madrid), Andres Iniesta (Barcelona), Sergio Busquets (Barcelona), Santi Cazorla (Malaga), Thiago Alcantara (Barcelona), Xavi (Barcelona), Javi Martinez (Athletic Bilbao).

Washambuliaji: David Silva (Manchester City), David Villa (Barcelona), Pedro (Barcelona), Fernando Torres (Chelsea), Fernando Llorente (Athletic Bilbao), Alvaro Negredo (Sevilla) pamoja na Juan Mata (Valencia).

No comments:

Post a Comment