KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 12, 2011

Tony Pulis AZUNGUMZIA USAJILI.


Meneja wa Stoke city Tonny Pulis amedhamiria kufanya usajili wa wachezaji sita kabla ya August 31 ambapo itakuwa mwisho wa harakati za usajili wa wachezaji katika bara zima la Ulaya.

Tonny Pulis amedhamiria kufanya hivyo kwa kutaka kuboresha kikosi chake ambacho msimu uliopita kilifanikiwa kutinga katika hatua ya fainali ya kombe la FA na kisha kikaambulia kisago cha bao moja kwa sifuri kutoka kwa Man city.

Hata yhivyo wachezaji wanne kati ya wachezaji sita wanaotakiwa huko Britannia Stadium wamefanya kuwa siri huku jina la mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Peter Crouch pamoja na kiungo Wilson Palacio yakianikwa hadharani na uongozi wa Stoke city.

Tonny Pulis amesema anaamini usajiliwa wa chezaji hao wawili kutoka Spurs utakamilishwa siku za hivi karibuni baada ya kuwasilishwa ofa nyingine kufuatia ofa ya mwanzo kuwekwa kapuni huko White Hart Lane.

Hata hivyo amedai kwamba usajili wa Peter Crouch pamoja na Wilson Palacio utakamilishwa kwa mazungumzo binafsi kati ya uongozi wa Spurs dhidi ya Stoke City.

Licha ya majina hayo kufanywa siri katika mtandao wa klabu ya Stoke City, baadhi ya mitandao imeripoti kwamba wachezaji wengine wanaowaniwa na klabu hiyo ni Jonathan Woodgate Matthew Upson pamoja na Joey Barton.

No comments:

Post a Comment