KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 24, 2011

UHOLANZI YAKAMATA USUKANI VIWANGO VYA UBORA WA SOKA DUNIANI.


Nchi ya Uholanzi imefanikiwa kupanda katika nafasi ya kwanza katika orodha ya viwango vya soka duniani ambayo hutolewa kila mwezi na shirikihso la soka ulimwenguni kote FIFA.

Uholanzi wamefanikiwa kupanda katika nafasi ya kwanza iliyokua inashikiliwa na nchi ya Hispania ambayo ndio bingwa wa dunia kupitia fainali za kombe la dunia zilizofanyika mwaka 2010 nchini Afrika kusini.

Kigezo kikubwa kilichotumiwa na FIFA kuipandisha kiwango nchi hiyo, ni hatua ya kufungwa kwa timu ya taifa ya Hispania katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki mwanzoni mwa mwezi huu dhidi ya timu ya taifa ya Italia iliyoibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Katika michezo hiyo ya kimataifa ya kirafiki, timu ya taifa ya Uholanzi haikucheza mchezo wake dhidi ya Uingereza, kufuatia ghasia zilizoibuka jijini London ambazo zilipelekea uongozi wa FA kutangaza kuuahirisha mchezo huo uliokua umepangwa kufanyika katika uwanja wa Wimbeley.

Kufautia hatua hiyo nchi ya Uholanzi inakuwa nchi ya saba kukamata usukani wa viwango vya ubora duniani toka ulipoanzishwa utaratibu huo mwaka 1993, ambapo tayari nchi kama Argentina, Brazil,Ufaransa, Ujerumani, Italia pamoja na Hispania zimeshafanikiwa kukamata namba moja.

Nao mabingwa mara tano wa dunia Brazil wameporomoka kwa nafasi mbili, na hii imesababishwa na hatua ya kukubali kichapo cha mabao matatu kwa mawili katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Ujerumani.

Kabla ya hapo nchi ya Brazil, ilikua katika nafasi ya nne na sasa imeporomoka hadi katika nafasi ya sita, huku nchi ya Uruguay, ikisalia katika nafasi ya tano na kuwa nchi ya kwanza kutoka ukanda wa bara la Amerika ya kusini.

Orodha ya viwango vya ubora wa soka duniani iliyotolewa hii leo na FIFA kwa upande wa nchi zilizokamata nafasi kumi za mwanzo.

1. (2) Netherlands

2. (1) Spain

3. (3) Germany

4. (6) England

5. (5) Uruguay

6. (4) Brazil

7. (8) Italy

8. (7) Portugal

9. (10) Argentina

10. (9) Croatia

No comments:

Post a Comment