KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 16, 2011

UPEPO WA CHELSEA KUMKIMBIZA Nicolas Anelka?

Mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Chelsea Nicolas Anelka huenda akaihama klabu hiyo kabla ya august 31 ambapo itakuwa mwisho wa dirisha la usajili katika kipindi hiki.

Nicolas Anelka ambae alijumuishwa kikosini mwishoni mwa juma lililopita katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza msimu huu, anafikiria kufanya hivyo kufuatia uhalisia wa upatikanaji wa nafasi ndani ya kikosi cha chelsea.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32, anakabiliwa na changamoto mbali mbali klabuni hapo kutokana na hatua ya kusajiliwa kwa Fernando Torres mwanzoni mwa mwaka huu, kurejea kwa mshambuliaji kinda Daniel Sturridge aliekua ametolewa kwa mkopo huko Bolaton wanderers pamoja na uwepo wa mshambuliaji mwingine Didier Drogba.

Taarifa zilizopo zinadai kwamba Nicolas Anelka anapewa nafasi ya kipekee ya kujiunga na Spurs ambao wapo tayari kuwaachia baadhi ya washambuliaji wao kama Jermain Defoe pamoja na Peter Crouch huku Robbie Keane akiwa tayari ameshajiunga na LA Galax usiku wa kuamkia hii leo.

Wakati huo huo Chelsea wapo mbioni kutuma ofa ya kutaka kumsajili kiungo kutoka nchini Ureno pamoja na klabu ya Liverpool Raul José Trindade Meireles kwa kiasi cha paund million 27.

Chelsea wanajiandaa kufanya hivyo baada ya kuona hakuna muelekeo wa kumpata kiungo kutoka nchini Croatia na klabu ya Tottenham Hotspurs Luca Modric ambae anawekewa ngumu ya kufunguliwa milango ya kuondoka huko White Hart Lene.

Meneja wa Chelsea Andre Villas-Boas, amempendekeza kiungo huyo kutokana na mazoea yaliopo kati yao ambapo kwa mara ya mwisho alimfundisha akiwa na Fc Porto nchini Ureno kabla ya kusajiliwa na Liverpool mwezi August mwaka 2010.

Raul José Trindade Meireles anafikiriwa huenda akaondoka Anfield kufuatia kusajiliwa kwa viuingo kama Jordan Henderson, Charlie Adam pamoja na winga Stewart Downing.

Katika hatua nyingine meneja wa Stoke City, Tony Pulis amemtetea muamuzi aliechezesha pambano la mwishoni mwa juma lililopita ambalo lilishuhudia kikosi chake kikilazimisha sare nyumbani dhidi ya Chelsea.

Amesema haoni sababu la kumlaumu muamuzi huyo kwa madai aliwanyima penati Chelsea zaidi ya mara mbili huku akitoa angalizo kwa mashabiki wa klabu hiyo kutazama mbele na kusahau yaliyopita.

Hata hivyo meneja huyo bado hakuacha kuendelea kukisifia kikosi cha Chelsea kwa kudai kina uwezo mzuri wa kiushindani msimu huu.

No comments:

Post a Comment