KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 2, 2011

USAJILI WA JUAN MATA KWENA ARSENAL WAKWAMA.

Baba mzazi wa kiungo wa kimataifa toka nchini Hispania, Juan Mata amesema bado anaamini washika bunduku wa Ashburton Grove Arsenal wana nafasi ya kipekee ya kumsajili mwanawe katika kipindi hiki cha kuelekea msimu mpya wa ligi.

Juan Manuel Mata Rodriguez, baba mzazi wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 ametoa mtazamo huo baada ya viongozi wa Arsenal kushindwa kuuwahi muda wa kukamilisha dili la uhamisho kama walivyopangiwa na viongozi wa Valencia hapo jana.

Baba huyo amesema mwanawe ana vigezo vyote vya kuitumikia klabu ya Arsenal na anaamini meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger ana mipango mizuri ya kukamilisha dili la uhamisho wake kabla ya kufungwa kwa mlango wa usajili August 31 mwaka huu.

Arsenal walitakiwa kufanya hima kumaliza dili la kumsajili Juan Mata, kabla ya siku ya jana kwa ada ya paund million 22, hatua ambayo inakwenda katika mipango tofauti ambayo huenda ikapandisha kiwango cha ada ya uhamisho wa mchezaji huyo.

Hata hivyo tayari Juan Mata ameshaonyesha dalili zote za kuwa tayari kusajiliwa na Arsenal, licha ya wapinzani wa klabu hiyo ya jijini London, Tottenham Hotspurs kutangaza vita ya kuingilia kati mipango hiyo.

Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kwamba kusajiliwa kwa Juan Mata huko Emirates Stadium kutatokana na mwenendo wa dili la uhamisho wa kiungo na nahodha wa Arsenal Cesc Fabregas, anaetakiwa kurejea FC Barcelona lakini uhamisho wake umegubikwa na wingu kubwa la kushindwa kuafikiwa kwa ada ya uhamisho.

No comments:

Post a Comment