KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 8, 2011

Wesley Sneijder AJINADI BINAFSI.


Kiungo wa kimataifa toka nchini Uholanzi, na klabu ya Inter Milan Wesley Sneijder bado anaendelea kujipa nafasi ya kucheza soka nchini Uingereza katika msimu mpya wa ligi ambapo kwa sasa amelazimika kupasua ukweli wa kinachoendelea huko Stadio Guissepe Meazza.

Wesley Sneijder amesema tayari ameshawekwa katika orodha ya wachezaji watakaouzwa klabuni hapo hivyo hatua hiyo inaifanya klabu ya Man utd pamoja na Man city kuendelea kuamini watampata kirahisi kabla ya August 31.

Amesema kwa sasa Inter Milan wanahitaji fedha na wameona ni bora wamuweke katika orodha hiyo kufuatia ushawishi unaendelea kutolewa na vilabu hivyo viwili vya mjini Manchester ambavyo vina kiu ya kufanya vyema katika msimu wa mwaka 2011-12.

Hata hivyo amedai kwamba katika siku tano ambazo atakua na timu ya taifa ya Uholanzi ambayo inajiandaa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi Uingereza, kila jambo litakua sawa, na mustakabali wa safari yake ya kuondoka mjini Milan itafahamika kwa asilimia 100.

Nae meneja wa Inter Milan Gian Piero Gasperini mwishoni mwa juma lililopita alikaririwa na vyombo vya habari akiwa nchini China, ambapo alisema mustakabali wa Wesley Sneijder, utaeleweka ndani ya juma hili.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, amekua katika mawindo ya kutaka kucheza nchini Uingereza toka alipoaanza kuhusishwa na taarifa za kutakiwa kuziba mwanya wa kiungo Paul Scholes ambae alitangaza kustahafu soka mwishoni mwa msimu uliopita.


Hata hivyo taarifa nyingine zinadai kwamba Man City hawana uhakika kama watamsajili Wesley Sneijder, kufuatia kauli iliyotolewa na Roberto Mancini ambayo imedhihirisha wazi kutokumuhitaji mchezaji anaecheza nafasi ya kiungo huko Etihad Stadium.

No comments:

Post a Comment